VIATU VYA HARUSI
Unapojiandaa kufanya sherehe ya harusi unashauriwa pia uandae mapema viatu kwa ajili ya siku hiyo maalumu katika maisha yako hii itakusaidia kuchagua kiatu utakachoona kinafaa kuna vitu mhimu unapaswa uvizingatie kwa ajili ya muonekano wako wa siku iyo vitu hivyo ni
- Uchague kiatu kitakachokufanya uwe huru katika kutembea hii inatokana na watu wengi kupenda kuvaa viatu virefu maarufu kwa jina la (high heels) siwatu wote wanaweza kutembea na viatu aina hiyo wengi hushindwa na hujikuta wakiumia bila wao kuelewa
- Usifuate mkumbo kwa kuvaa usichoweza kumudu katika kutembea wengine hufuata mkumbo wa marafiki zao ambao huwashauri na kuwachagulia viatu hivyo
- Kubali kuonekana mshamba kwa kuckukua viatu vifupi ili uwe huru kuliko kuonekana mjanja wa kuvaa kiatu kirefu huku ukiwa mshamba wa kutembelea kwani itawafanya watu wakuone kama mshamba na pia hujitambui
- Kwa wale wanaofanya sherehe wakiwa na ujauzito wanashauriwa kuvaa viatu visivyo virefu ili wasiumize watoto wao walioko tumboni au kuwasababishia matatizo makubwa wakati kujifungua kwani si vizuri kuvaa viatu ukiwa katika hali hiyo.
- Kwa wanaume wanashauriwa kuchagua viatu vitakavyowafanya kuonekana tofauti na walivyozoeleka pia viendane na nguo zao
Zifuatazo ni picha mbali mbali za viatu
No comments:
Post a Comment