KWA MAONI AU USHAURI TUMA KWA E-mail: lovenessbernard@gmail.com

Thursday, April 17, 2014

WAPAMBE WA HARUSI

                    MAVAZI YA WAPAMBE WA HARUSI

Hiki ni kitu mhimu sana cha kuzingatia unapojiandaa kufanya sherehe yako mavazi ya wapambe yachaguliwe mapema ikiwemo kujua rangi yake na kushonwa mapema kuepusha usumbufu kwa siku hiyo maalum kwani kinaweza tokea kitu chochote kama vile nguo kubana au kupwaya  kama itaandaliwa mapema itarekebishwa mapema kuliko siku ya tukio lenyewe.

Aidha unapaswa uchague nguo ambazo zitawasitiri vema wapambe kwani kwa siku  hiyo iwe kanisani au ukumbini kuepusha  kero ambazo siku hizi zinajitokeza kwa wapambe kufukuzwa kanisani au kucheleweshwa kwa misa ya ndoa hiyo kutokana na padri au mchungaji kukerwa na mavazi ya harusi hiyo.

Kulingana na mila na desturi zetu mavazi mazuri ni yale ya kusitiri mwili  aidha yatawafanya wawe huru na kuifanya harusi yako kusemwa kwa uzuri na kuwa mfano bora wa kuigwa na siyo kuwa mfano wa harusi mbaya,japo kuna fasheni mbalimbali nguo ziwe za kustiri maungo kama vile sehemu za kifua na mapaja sababu vinaweza kuwaondolea waalikwa usikivu na kubaki wakiwaangalia wapambe au kuwaona kama watu wasiona maadili .

Japo siku hizi kuna utandawazi ni mhimu pia kuzingatia maadili yetu siyo kuiga kila kitu kutoka mataifa mengine, suala hili la mavazi linalalamikiwa sana na wapambe wa kike(wadada) ndio wanaovaa vibaya tofauti na wakaka ambao hupendeza sana .

Wamependeza kweli kweli kwa mpangilio mzuri wa rangi

 Mhhhh! kwa pozi hili la wapambe na nouma kwelikweli


 Mtoto wa raisi wa Nigeria akiwa na wapambe wake siku ya harusi yake





 Harusi ikiwa na wapambe wamependeza kwelikweli


 Angalia rangi ya bluu ikitumika kama kama rangi ya harusi inapendeza kweli












1 comment: